Widgets

WANAHITAJIKA VIJANA 31 KUJAZA NAFASI ZA AJIRA SERIKALINI

Wednesday, August 27, 2014 Unknown 0 Comments



OFISI YA RAIS - SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/G/55
26 Agosti, 2014
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa
mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa
na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki,
pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea
katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya
Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi 31 kwa ajili ya Katibu Mkuu
Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
i. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
ii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua za maombi ya nafasi za kazi
kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iii. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili
kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
iv. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
v. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato
cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu
2
mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe
sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vi. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za
kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
vii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
viii. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa
kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
ix. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika
utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
x. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria.
xi. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 11 September, 2014
xii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira
HAURUHUSIWI.
xiii. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe
kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Katibu,
AU
Secretary,
Sekretariati ya Ajira katika
Public Service Recruitment
Utumishi wa Umma,
Secretariat,
SLP.63100,
P.O.Box 63100
Dar es Salaam.
Dar es Salaam.
3
1.0 AFISA MAMBO YA NJE DARAJA LA II (SECOND SECRETARY) – NAFASI 10
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa
Kimataifa.
1.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kuandaa Muhtasari, nakala na taarifa zinazohusu masuala ya kimahusiano ya
kimataifa.
· Kuhudhuria mikutano mbalimbali.
· Kuandaa mahojiano.
· Kufuatilia masuala mbalimbali ya kimataifa.
· Kufanya utafiti juu ya masuala mbalimbali yanayohusu uchumi, siasa na jamii.
· Kutunza kumbukumbu za matukio mbalimbali.
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye Shahada ya Sanaa (B.A) ambao wamejiimarisha (major) katika
fani ya uhusiano wa Kimataifa (international Relations), Sheria au Uchumi kutoka
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
Aidha, wawe wamefanya na kufaulu mtihani unaotolewa Chuo cha Diplomasia,
Dar es Salaam.
1.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
2.0 KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III (PERSONAL SECRETARY GRADE III) –
NAFASI 11
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa
Kimataifa.
2.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida.
· Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu
wanapoweza kushughulikiwa.
· Kusaidia kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao,
safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa wakati unaohitajika.
· Kusaidia kutafuta na kumpatia Mkuu wake majadala, nyaraka au kitu chochote
kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini.
· Kusaidia kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia
kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.
· Kusaidia kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa walio katika sehemu alipo, na
kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
· Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi.
4
2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV waliohudhuria Mafunzo ya Uhazili na kufaulu
mtihani wa Hatua ya Tatu. Wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili na
Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na wawe wamepata mafunzo ya
Kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata cheti
katika programu za Window, Microstoft Office, Internet, E-mail na Publisher.
2.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa mwezi.
3.0 AFISA UTUMISHI DARAJA LA II (HUMAN RESOURCES OFFICER GRADE II) –
NAFASI 1
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa
Kimataifa.
3.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kutunza Kumbukumbu sahihi za watumishi wote katika Wizara, Mikoa, Wilaya na
Idara zinazojitegemea kulingana na mahali alipo.
· Kutafsiri na kushughulikia utekelezaji wa miundo ya utumishi.
· Kutafiti, kuchanganua na kukadiria idadi ya watumishi wanaohitaji mafunzo.
· Kuandaa na kupanga mipango ya mafunzo ya muda mfupi na mrefu.
· Kukadiria na kupanga mahitaji ya vifaa vya mafunzo kwa kushirikiana na vyuo
vilivyopo chini ya sekta zinazohusika.
· Kukusanya, kuchambua na kupanga takwimu na kumbukumbu zote zinazohusu
mipango ya watumishi.
3.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Sayansi Jamii au Sanaa kutoka katika
Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali ambao wamejiimarisha (major) katika
mojawapo ya fani zifuatazo:-
§ Menejimenti ya Raslimali Watu (Human Resources Management).
§ Elimu ya Jamii (Sociologly).
§ Utawala na Uongozi (Public Administration).
· Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta
3.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
5
4.0 MPOKEZI (RECEPTIONIST) – NAFASI 4
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa
Kimataifa.
4.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kupokea wageni na kuwasaili shida zao.
· Kutunza rejesta ya wageni wa ofisi na kufanya uchambuzi wa wageni wanaoingia
ili kutoa ushauri juu ya utaratibu bora wa kupokea wageni.
· Kupokea na kusambaza maombi ya simu za ndani.
· Kutunza na kudumisha usafi wa “Switchboard” na ofisi zake.
· Kuwaelekeza wageni wa ofisi kwa maafisa/ofisi watakakopewa huduma.
· Kuhakikisha kwamba wageni wanaoingia ndani wanamiadi (Appointment) au
wamepata idhni ya maafisa husika.
· Kupokea simu kutoka nje na kuzisambaza kwa maofisa mbalimbali ofisini.
· Kupokea simu kutoka “Extension” za ndani na kupiga nje ya ofisi.
· Kutunza rejesta ya simu zinazopokelewa kutoka nje ya ofisi na zinazopigwa
kwenda nje.
4.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha IV waliofaulu masomo ya Kiingereza, Kiswahili
na Hisabati na kufuzu mafunzo ya Mapokezi na Upokeaji Simu kutoka vyuo
vinavyotambuliwa na Serikali.
4.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa mwezi
5.0 MSAIDIZI WA OFISI (OFFICE ASSISTANT) – NAFASI 5
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa
Kimataifa.
5.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kufanya usafi wa ofisi na mazingira ya nje na ndani ikiwa ni pamoja na kufagia,
kufuta vumbi, kupiga deki, kukata majani, kupalilia bustani, kumwagilia maji
bustani, kupanda maua au miti na kusafisha vyoo.
· Kuchukua na kupeleka majalada na hati nyingine kwa maofsa waoaohusika na
kuyarudisha sehemu zinazohusika.
· Kusambaza barua za Ofisi kama jinsi atakavyoelekezwa.
· Kutayarisha chai ya ofisi.
· Kupeleka mfuko wa posta na kuchukua barua kutoka Posta.
· Kuhakikisha kwamba vifaa vya ofisi vinaweka sehemu zinazostahili.
· Kufungua Milango na Madirisha ya Ofisi wakati wa Asubuhi na Jioni kuyafunga
baada ya Saa za Kazi.
6
· Kudurufu barua au machapisho kwenye mashine za kudurufia.
· Kuweka katika majalada nakala za barua zilizochapwa katika ofisi walizomo.
· Kutunza vifaa vya ofisi na kutoa ripoti kila vinapoharibika.
5.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliofaulu vizuri katika masomo ya
Kiingereza, Kiswahili na Hisabati.
5.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi.
X.M. DAUDI
Katibu
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.