Kuhusu Blog

Monday, August 11, 2014 Unknown 0 Comments

Ajira kwa vijana imekua ni changamoto kubwa hapa nchini na Africa kwa ujumla. Tanzania Ikiwa na moja ya tatu ya vijana kwenye idadi yote ya watu Tanzania, takwimu zinaonyesha vijana ndio wana athirika sana na kuongezeka kwa ukosefu wa ajira kuliko makundi mengine. 

Blog ya Ajira – Kijana wa leo inalenga katika kuwaelimisha vijana kwa nia ya kuwakwamua vijana kimaisha kupitia ujasiliamali na kujiajiri wenyewe. 

Ili kuongeza ajira, inabidi tutengeneze ajira wenyewe kuliko kusubiri kuajiriwa. Uhakika wa ajira upo kama utajitengenezea ajira yako mwenyewe. Takwimu zinaonyesha katika vijana 1000 ni asilimia 14 tu ndio wana ajira rasmi yenye mshahara.

Posts zetu zinalenga sio tu katika kuwapa mbinu mbali za ufundi/ujuzi (technical skills) wa ujasiriamali pia fikra za kiujasiriamali kwa kuwahamasisha, kuwaelimisha na kuwashauri. 

Lengo letu (mission/vision) ni Kuwahamasisha vijana wawe wawajibikaji, wenye nia ya kujikwamua kimaisha na wenye mchango kwenye jamii.

Kwenye blog yetu ya ajira-kijana wa leo, tunakaribisha watu wote wa rika zote wenye mawazo, wanaotaka kujifunza na kuchangia kwa namna yeyote endelevu kwa kuwa ni wazi ya kwamba ili kuongeza mafanikio, usawa, na utulivu katika jamii yetu, ni lazima tuwawezeshe kikamilifu vijana ambao ni hazina kubwa ya nchi ambayo haitumiki ipasavyo katika fursa za ujasiriamali na uzoefu kuhakikisha kwamba vijana wote wanapata nafasi ya kuendeleza vipaji vyao na kutimiza ndoto zao.