MAKALA.:CHANGAMOTO ZA AJIRA
VIJANA WALIO JITOKEZA KUOMBA KAZI HIVI KARIUNI |
Nchini Tanzaia wengi wa vijana wamekuwa wakiilalamikia Serikali yao ya kwamba imekosa mipango muhimu ya kuwawezesha vijana na kuwatengenezea mazingira ya wao kujiajiri, changamoto ya mifumo ya elimu inaonekena kuwa kikwazo katika kufikia malengo yao.
Maafisa wa nchi za Kiafrika walioshiriki Kongamano la Ukosefu wa Ajira na Madhara yake Barani Afrika lililofanyika katika mji mkuu wa Senegal, Dakar wametahadharisha juu ya matokeo mabaya ya kukosa ajira vijana. Wamesema kuwa, idadi kubwa ya vijana barani humo hawana kazi, suala ambalo ni hatari kubwa kwa amani na utulivu wa bara hilo.
Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, watu milioni 200 miongoni mwa wakazi wa Afrika ni vijana wenye umri kati ya miaka 15 na 24. Hii ni katika hali ambayo Umoja wa Mataifa unasema kuwa, idadi ya vijana wasio na ajira barani Afrika ni mara mbili zaidi ya watu wazima. Ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana unawafanya washawishike kujiunga na makundi yenye misimamo mikali. Mfano wa hali hiyo unashuhudiwa katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Nigeria na Mali. Makundi yenye mitazamo ya kufurutu ada nchini Mali mwaka 2012 yalidhibiti kwa miezi kadhaa eneo la kaskazini mwa nchi hiyo. Hivi sasa pia eneo hilo bado linasumbuliwa na machafuko na ukosefu wa amani.
Inaonekana kuwa, vijana wasio na ajira ni mawindo mazuri kwa makundi yenye kufurutu ada na yanawashawishi kujiunga nao kwa kiasi kidogo tu cha fedha. Nchini Nigeria pia ukosefu wa ajira, umaskini na kubaguliwa Waislamu waliowengi, ni miongoni wa sababu zinazowafanya vijana wajiunge na kundi lenye misimamo mikali la Boko Haram. Licha ya pato la mafuta, lakini karibu asilimia 70 ya wananchi wa Nigeria wanaishi chini ya mstari wa umasikini. Hii ni katika hali ambayo hali ya maisha ya Wakristo waliowachache nchini humo ni nzuri zaidi ikilinganishwa na ya Waislamu, na wao ndio wanaofaidika zaidi na pato la maliasili na utajiri wa nchi hiyo.
Kwa utaratibu huo tunaweza kusema kuwa, kukosa matumaini ya kuboreka hali ya kiuchumi ya vijana na utendaji mbovu wa serikali ndiyo sababu kuu ya kujiunga na makundi yenye kufurutu ada. Hali hiyo hiyo pia inashuhudiwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ambapo ukosefu mkubwa wa ajira umesababisha kuendelea migogoro nchini humo.
Kwa kutilia maana ukweli huo baadhi ya weledi wa mambo wanaamini kuwa, matokeo ya kukosa kazi kwa vijana ni hali inayoshuhudiwa hivi sasa barani Afrika.
Kwa miaka kadhaa mtawalia, mitazamo ya kikoloni imekuwa sababu ya kukosekana maendeleo katika nyanja mbalimbali barani Afrika. Wakati huo huo kukaririwa mapinduzi ya kijeshi, serikali fisadi na vibaraka vimezorotesha na kudumaza uchumi wa nchi za Afrika. Inaonekana kuwa, ni vigumu kupunguza kiwango cha watu wasiokuwa na ajira huku nchi nyingi za Kiafrika zikiendelea kukabiliwa na hali mbaya ya kisiasa na kiuchumi.
Wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa, vijana wanapaswa kusaidiwa sambamba na kubadilisha hali ya sasa, ili kuandaliwe mustakbali mzuri zaidi katika bara hilo, suala linalopaswa kupewa kipaumbelea na serikali za nchi za Kiafrika.
Blog hii pamoja na kukupa habari, makala mbalimbali na changamoto za ajir nchini itakuwa inatoa matangazo ya kazi na watu mbalimbali waliobuni vitu mbalimbali na kujiajiri wenyewe na kujiingizia kipato cha uhakika bila kusubiri kuajiriwa.