NAFASI ZA AJIRA 102
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA
UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/H/03
25 Septemba, 2014
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Sekretariati ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwamujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa
na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, chombo hiki,
pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza nafasi wazi za kazi zinazotokea
katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya
Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 102 za kazi kwa ajili ya Katibu Mkuu
Wizara ya Maji,
NB: MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za
kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe juu ya bahasha, kutozingatiwa hili
kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees)
watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kidato
cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu
mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe
sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
vii. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za
kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
viii. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na
kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa
kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika
utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika
Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za
kisheria.
xii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 8 Oktoba, 2014
xiii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira
HAURUHUSIWI.
xiv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe
kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Katibu,
AU
Secretary,
Sekretariati ya Ajira katika
Public Service Recruitment
Utumishi wa Umma,
Secretariat,
SLP.63100,
P.O.Box 63100
Dar es Salaam.
Dar es Salaam.
1.0
FUNDI SANIFU MSAIDIZI (UPIMAJI ARDHI) - (ASSISTANT WATER WORKS
TECHNICIAN GEOMETRIC) – NAFASI 25-ZINARUDIWA
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
1.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kufanya kazi kwa kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi Sanifu aoyesajiliwa ili
aweze;
Kushirikiana na Wahandisi wa Maji na kuwaongoza walengwa katika kuchagua njia za
kupitisha bomba kwa ajili ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
Kupima hali ya kijiografia ya maeneo ya inayokusudiwa kujengwa au yenye miradi ya
maji na usafi wa mazingira ili kuwezesha usanifu wa miundo mbinu miradi;
Kupima uwekaji wa vifaa vya miundo mbinu kwenye ardhi wakati wa ujenzi wa miradi ya
maji na usafi wa mazingira;
Kunakili na kutunza taarifa za upimaji wa ardhi kwa ajili ya miundo mbinu ya miradi ya
maji na usafi wa mazingira kwa namna inayokubalika kwa mchoraji wa ramani za usanifu
wa miradi kufanya kazi yake kwa unadhifu;kuchora ramani za maeneo ya miradi ya maji
na usafi wa mazingira kwa namna zote zinazokubalika kwa ajili ya kuwezesha usanifu
wa miundo mbinu ya maji na usafi wa mazingira;
Kumsaidia Fundi Sanifu katika kazi za upimaji ardhi.
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka
mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachitambuliwa na Serikali ambao
wana Cheti cha ufundi Daraja III (Water Works Technician Geometric).
1.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
2.0
FUNDI SANIFU MSAIDIZI MITAMBO YA MAJI (PAMPU) – NAFASI 25-ZINARUDIWA
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
2.1 MAJUKUMU YA KAZI
Atafanya kazi kwa kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi Sanifu aliyesajiliwa ili
aweze;
Kufunga pampu na injini za aina mbalimbali za miradi ya maji na usafi wa mazingira;
Kufanya usafi na ukaguzi wa pampu na injini za miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa
ajili ya kukidhi uendeshaji nadhifu, endelevu na kuzuia uharibifu;
Kuhudumia uendeshaji wa pampu na injini za miradi ya maji;
Kufanya matengenezo ya kawaida, ya vipindi na ya kuzuia uharibifu wa pampu na injini
kwa kufuata miongozo ya uendeshaji na matengenezo na inapohitajika kwa dharura;
Kunakiri, kutayarisha, kukusanya, kutunza na kuziwasilisha takwimu za uendeshaji na
matengenezo ya pampu na injini za miradi ya maji;
Kumsaidia Fundi Sanifu katika kazi za kiufundi.
2.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka
mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachitambuliwa na Serikali ambao
wana Cheti cha ufundi Daraja III (Mitambo Ya Maji (Pampu).
2.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
1.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI MITAMBO YA MAJI (UMEME) – NAFASI 25-ZINARUDIWA
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
1.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kufanya kazi kwa kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi sanifu aliyesajiliwa ili aweze;
Kufunga mfumo wa umeme unaohitajika kwa ajili ya uendeshaji wa mitambo ya miradi ya
maji na usafi wa mazingira;
Kufunga mota na vifaa vingine vya umeme vya aina mbalimbali vya miradi ya maji na
usafi wa mazingira;
Kufanya usafi na ukaguzi wa mfumo wa umeme, mota na vifaa vingine umeme vya miradi
ya maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya kukidhi uendeshaji nadhifu wa pampu na
kuzuia uharibifu;
Kuendesha mitambo inayotumia umeme ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
Kufanya matengenezo ya kawaida, ya vipindi na ya kuzuia uharibifu kwenye mfumo wa
umeme, mota na vifaa vingine umeme kwa kufuata miongozo ya uendeshaji, na
inapohitajika kwa dharura.
Kunakili, kutayarisha, kukusanya, kutunza na kuziwasilisha takwimu za uendeshaji na
matengenezo ya mitambo inayotumia umeme ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
Kumsaidia Fundi Sanifu katika kazi za kiufundi.
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka
mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachitambuliwa na Serikali ambao
wana Cheti cha ufundi Daraja III (Plants Technician Electrical).
1.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
3.0
FUNDI SANIFU MSAIDIZI - (ASSISTANT TECHNICIAN WELDING) NAFASI 2-
ZINARUDIWA
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
1.4 MAJUKUMU YA KAZI
Kufanya kazi kwa kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi Sanifu aliyesajiliwa ili aweze;
Kufunga pampu na injini za aina mbalimbali za miradi ya maji na usafi wa mazingira;
Kufanya usafi na ukaguzi wa pampu na injini za miradi ya maji na usafi wa mazingira kwa
ajili ya kukidhi uendeshaji nadhifu, endelevu na kuzuia uharibifu;
Kuhudumia uendeshaji wa pampu na injini za miradi ya maji;
Kufanya matengenezo ya kawaida, ya vipindi nay a kuzuia uharibifu wa pampu na injini
kwa kufuata miongozo ya uendeshaji na matengenezo na inapohitajika kwa dharura;
Kunakili, kutayarisha, kukusanya, kutunza na kuziwasilisha takwimu za uendeshaji na
matengenezo ya pampu na injini za miradi ya maji;
Kumsaidia Fundi Sanifu katika kazi za kiufundi.
1.5 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka
mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachitambuliwa na Serikali ambao
wana Cheti cha ufundi Daraja III katika fani ya Welding na fiter turner.
1.6 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
4.0
FUNDI SANIFU MSAIDIZI (UFUNDI BOMBA) - (ASSISTANT WATER WORKS
TECHNICIAN PLUMBING) – NAFASI 1-INARUDIWA
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
1.7 MAJUKUMU YA KAZI
Kufanya kazi kwa kuongozwa na chini ya uangalizi wa Fundi Sanifu aliyesajiliwa ili aweze;
Kufunga mitandao ya bomba za aina mbalimbali ya miradi ya maji na usafi wa mazingira;
Kufanya usafi na ukaguzi wa mitandao ya bomba ya miradi ya maji na usafi wa mazingira
kwa ajili ya kukidhi uendeshaji nadhifu, endelevu na kuzuia uharibifu;
Kuwezesha uzalishaji na usambazaji wa maji na utoaji wa majitaka kwa kupitia mitandao
ya bomba za miradi ya maji na usafi wa mazingira.
Kufanya matengenezo ya kawaida ya vipindi nay a kuzuia uharibifu wa mitandao ya
bomba kwa kufuata ratiba na inapohitajika kwa dharura.
Kunakili, kutayarisha, kukusanya, kutunza na kuziwasilisha takwimu za uendeshaji na
matengenezo ya mitandao ya bomba za miradi ya maji na usafi wa mazingira;
Kumsaidia Fundisanifu kazi za kiufundi.
1.8 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka
mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachitambuliwa na Serikali ambao
wana Cheti cha ufundi Daraja III (Plumbing).
1.9 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
5.0
MHANDISI DARAJA LA II (MAJI) – WATER RESOURCE ENGINEER –
NAFASI 14-INARUDIWA
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
5.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kushughulikia upembuzi yakinifu, usanifu wa ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya
miundombinu midogo midogo ya usambazaji maji na kushiriki shughuli za upembuzi
yakinifu, usanifu, ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya miundombinu mikubwa ya
ujenzi wa usambazaji maji na usafi wa mazingira.
Kufanyia mapitio taarifa za upembuzi yakinifu na sanifu za ujenzi wa miundombinu ya
miradi ya usambazaji maji na usafi wa mazingira.
Kufanyia ukaguzi wa utekelezaji wa ujenzi, uendeshaji na utengenezaji wa miundombinu
ya uzalishaji na usambazaji maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya kupata ubora
unaokusudiwa.
Kushiriki katika kazi ya kupendekeza miradi na kupitia mapendekezo ya miradi (project
proposal) ya usambazaji maji na usafi wa mazingira.
Kufanya uchunguzi kuhusu uharibifu wa miundombinu au ajali zinazojitokeza wakati wa
utekelezaji wa miradi ya maji na usafi wa mazingira.
Kutayarisha bajeti ya utekelezaji wa shughuli za sekta za maji.
Kusimamia kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa ujenzi, uendeshaji na mategenezo ya
miundombinu ya miradi ya maji na usafi wa mazingira.
Kukusanya na kutayarisha taarifa mbalimbali za utekelezaji wa shughuli za sekta ya maji
kwa ajili ya matumizi ya sekta na kwa ajili ya kujisajili katika bodi ya Wahandisi.
5.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu ya uhandisi wa Maji (Water Resource
Engineering) kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.
5.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
6.0
MHANDISI DARAJA LA II (MAJI) – WATER RESOURCE WITH GIS ENGINEER –
NAFASI 4-INARUDIWA
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji.
6.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kushughulikia upembuzi yakinifu, usanifu wa ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya
miundombinu midogo midogo ya usambazaji maji na kushiriki shughuli za upembuzi
yakinifu, usanifu, ujenzi, uendeshaji na matengenezo ya miundombinu mikubwa ya
ujenzi wa usambazaji maji na usafi wa mazingira.
Kufanyia mapitio taarifa za upembuzi yakinifu na sanifu za ujenzi wa miundombinu ya
miradi ya usambazaji maji na usafi wa mazingira.
Kufanyia ukaguzi wa utekelezaji wa ujenzi, uendeshaji na utengenezaji wa miundombinu
ya uzalishaji na usambazaji maji na usafi wa mazingira kwa ajili ya kupata ubora
unaokusudiwa.
Kushiriki katika kazi ya kupendekeza miradi na kupitia mapendekezo ya miradi (project
proposal) ya usambazaji maji na usafi wa mazingira.
Kufanya uchunguzi kuhusu uharibifu wa miundombinu au ajali zinazojitokeza wakati wa
utekelezaji wa miradi ya maji na usafi wa mazingira.
Kutayarisha bajeti ya utekelezaji wa shughuli za sekta za maji.
Kusimamia kuratibu na kufuatilia utekelezaji wa ujenzi, uendeshaji na mategenezo ya
miundombinu ya miradi ya maji na usafi wa mazingira.
Kukusanya na kutayarisha taarifa mbalimbali za utekelezaji wa shughuli za sekta ya maji
kwa ajili ya matumizi ya sekta na kwa ajili ya kujisajili katika bodi ya Wahandisi.
6.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu ya uhandisi wa Maji (Water Resource with
GIS) kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali.
6.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
7.0
MHANDISI KILIMO DARAJA LA II (AGRO – ENGINEERS) – NAFASI 6-INARUDIWA
7.1 MAJUKUMU YA KAZI
Kuandaa program za mafunzo kwa wakulima kutumia zana za kilimo,
Kushiriki katika kufundisha wakulima na matumizi bora ya zana,
Kushiriki kutengeneza michoro/ramani za umwagiliaji,
Kushiriki katika ujenzi wa miradi ya umwagiliaji,
Kushirikiana na mafundi sanifu kuwafunindisha wakulima uendeshaji wa skimu
za umwagiliaji,
Kukusanya takwimu za miradi ya umwagiliaji,
Kushiriki kuratibu na kutoa huduma za umwagiliaji kwa vikundi vya umwagiliaji
pamoja na matumizi ya maji,
Kuandaa mafunzo/maonyesho ya matumizi ya za za kilimo,
Kufuatilia program za mafunzo ya wanyama kazi, mafundi wa matrekta na
wakulima jinsi ya matumizi ya wanyama na matrekta,
Kuwafundisha wakulima ujenzi wa vihengo bora na
Kushughulikia ubora wa zana na kuwashauri waagizaji na watengenezaji
ipasavyo.
7.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza (Bachelor Degree) ya uhandisi yenye
mwelekeo mkubwa katika fani ya Kilimo cha umwagiliaji na cha zana kutoka
Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali.
7.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS E Kwa
mwezi.
X.M. DAUDI
Katibu
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma.